| Swahili
UTURUKI
1 dk kusoma
Uturuki, Saudi Arabia zajadiliana usalama wa kikanda
Kulingana na vyanzo ndani ya wizara hiyo, wawili hao walijadili hali ya usalama wa kikanda, hususani mashambulizi dhidi ya Saudi Arabia.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Hakan Fidan amefanya mazungumzo ya simu na waziri mwenzake wa Saudia Arabia, Prince Faisal bin Farhan, yanayohusu masuala ya usalama wa kikanda.

Kulingana na vyanzo ndani ya wizara hiyo, wawili hao walijadili hali ya usalama wa kikanda, hususani mashambulizi dhidi ya Saudi Arabia.

Mazungumzo hayo, yanakuja wakati hali ya sintofahamu ikiendelea katika eneo la Mashariki ya Kati, ambapo waasi wa Kihouthi wameshambulia sekta ya nishati na viwanja vya ndege vya Saudi Arabia.

Toka mwaka 2015, Saudi Arabia imeongoza umoja wa nchi za Kiarabu dhidi ya Wahouthi.

CHANZO:Anadolu Agency