Rais Luiz Inacio Lula da Silva ametimiza miaka 81 siku ya Jumanne, na kuahidi kufanya kazi saa 24, baada ya kuchaguliwa tena kuliongoza taifa hilo wa muhula wa nne.
"Nitafanya kazi zaidi ya kiongozi mwingine yeyote aliyepita kwenye historia ya nchi hii," alisema, huku akiongeza kuwa atajitahidi kufanya kazi saa 24 kuhakikisha kuwa, Brazil inakuwa nchi bora kwa kila mtu.
Alipoulizwa kuhusu umri wake, Lula aliweka bayana kuwa, yuko vizuri kiafya, akiendelea kufanya mazoezi ya mwili kama kawaida.
Akizungumza katika hotuba ya moja kwa moja jijini Sao Paulo kufuatia ushindi wake, Lula ameahidi kushirikiana na Bunge lenye mwelekeo wa kihafidhina lililochaguliwa na wananchi, na kuhakikisha ushiriki mpana zaidi wa umma katika mchakato wa kufanya maamuzi.
















