Uturuki itaendelea kukuza ushirikiano na mataifa ya Kiturki, Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Hakan Fidan amesema.
Fidan alitoa kauli hiyo, kupitia jukwaa la X, mara baada ya kikao cha Mawaziri wa Mambo ya Nje wa mataifa ya Kiturki, kabla mkutano wa wakuu wa nchi hizo ulioandaliwa na Rais Recep Tayyip Erdogan.
“Ni matumaini yangu kuwa, mkutano huu utaleta baraka kwa nchi zetu,” alisema Fidan.
Kulingana na Fidan, mazungumzo yao yaliegemea umoja na mshikamano wa nchi hizo.
Mkutano wa Ankara kuangazia umoja na mshikamano
Mkutano huo, ambao utafanyika siku ya Alhamisi na Ijumaa, chini ya Kauli Mbiu ya Karne ya Kiturki: Umoja wa Lugha, Mawazo na Matendo.
Mkutano huo unatarajiwa kuwaleta pamoja viongozi kutoka nchi wanachama na wawakilishi wengine.
Nchi wanachama watano
Ukiwa umeanzishwa mwaka 2009 kama Baraza la Kiturki, taasisi hiyo ilibadili jina lake wakati wa kikao cha nane jijini Istanbul mwaka 2021.
Unaundwa na Uturuki, Azerbaijan, Kazakhstan, Uzbekistan na Kyrgyzstan.
Kwa upande wao, Turkmenistan, Hungaria, na Jamhuri ya Uturuki iliyopo Kaskazini mwa Cyprus wanahudhuria kama watazamaji.






















