| Swahili
UTURUKI
1 dk kusoma
Trump ampigia simu Erdogan, amtakia heri ya mkutano wa Kiturki
Wakati wa mazungumzo hayo, Trump alimtakia kila la heri Erdogan, kuelekea mkutano wa Umoja wa Nchi za Kiturki (OTS), kulingana na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki.
Trump ampigia simu Erdogan, amtakia heri ya mkutano wa Kiturki
Wakati wa mazungumzo hayo, Erdogan alimjulisha Trumo kuwa Ankara itakuwa mwenyeji wa mkutano wa 13 wa OTS

Rais Donald Trump wa Marekani amempigia simu Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa maalumu kwa ajili ya kuadhimisha siku ya Jamhuri ya Uturuki.

Wakati wa mazungumzo hayo, Trump alimtakia kila la heri Erdogan, kuelekea mkutano wa Umoja wa Nchi za Kiturki (OTS), kulingana na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki.

Kwa upande wake, Erdogan alimtumia Trump salamu kutoka kwa viongozi wa wanaohudhuria chakula hicho cha jioni.

Wakati wa mazungumzo hayo, Erdogan alimjulisha Trump kuwa Ankara itakuwa mwenyeji wa mkutano wa 13 wa OTS, ambapo viongozi hao wanatarajiwa kufanya maamuzi kuhusu umoja huo.

Kulingana na Erdogan, umoja huo utakuwa ni kielelezo cha utulivu katika eneo la Asia ya Kati.

 

CHANZO:TRT World and Agencies