| Swahili
ULIMWENGU
1 dk kusoma
Meya wa Japan aliyezimia kwa muda mrefu ‘afukuzwa kazi’
Kulingana na baraza hilo la madiwani, uamuzi huo umefikiwa ili kuepuka kuvuruga utekelezwaji wa majukumu ya kila siku ndani ya halmashauri ya jiji hilo.
Meya wa Japan aliyezimia kwa muda mrefu ‘afukuzwa kazi’
Hatakeyama alipoteza kumbukumbu kuanzia mwezi wa Februari mwaka huu baada ya kufanyiwa upasuaji.

Baraza la madiwani la Akita nchini Japan, limepiga kura ya kumuondoa madarakani Meya wa Jiji la Hachirogata Kikuo Hatakeyama, ambaye alikuwa amezimia kwa muda mrefu baada ya kupata changamoto kwenye ubongo wake.

Kura hiyo iliyopigwa siku ya Ijumaa, itamuweka nje ya madaraka Hatakeyama kuanzia Mei 19, kulingana na sheria za jiji hilo.

Kulingana na baraza hilo la madiwani, uamuzi huo umefikiwa ili kuepuka kuvuruga utekelezwaji wa majukumu ya kila siku ndani ya halmashauri ya jiji hilo.

Wakati huo huo, uchaguzi wa mrithi wake, unatarajiwa kufanyika ndani ya kipindi cha siku 50.

Hatakeyama alipoteza kumbukumbu kuanzia mwezi wa Februari mwaka huu baada ya kufanyiwa upasuaji.

CHANZO:AA