| Swahili
ULIMWENGU
1 dk kusoma
Sri Lanka yamshikilia mke rais wa zamani wa nchi hiyo kwa ufisadi
Shiranthi, ambaye ni mke wa kiongozi wa zamani wa nchi hiyo, Mahinda Rajapaksa, alifikishwa mbele ya mahakama ya jijini Colombo, akidaiwa kujipatia Dola za Kimarekani 30, 250 kutoka benki moja.
Sri Lanka yamshikilia mke rais wa zamani wa nchi hiyo kwa ufisadi
Mke wa rais wa zamani wa Sri Lanka, Shiranthi Rajapaksa amekamatwa siku ya Jumatano, akituhumiwa kwa ufisadi.

Mke wa rais wa zamani wa Sri Lanka, Shiranthi Rajapaksa amekamatwa siku ya Jumatano, akituhumiwa kwa ufisadi.

Shiranthi, ambaye ni mke wa kiongozi wa zamani wa nchi hiyo, Mahinda Rajapaksa, alifikishwa mbele ya mahakama ya jijini Colombo, akidaiwa kujipatia Dola za Kimarekani 30, 250 kutoka benki ya National Savings, kwa ajili ya kukabidhi mashine ya CT  kwa hospitali moja ya watoto nchini humo.

Inadaiwa kuwa, Shiranthi alishindwa kukabidhi mashine hiyo, akitumia pesa hizo kwa manufaa yake binafsi.

Jaji wa mahakama hiyo, aliamuru Shiranthi aendelee kukaa rumande, hadi Oktoba 13.

Mwenyekiti wa zamani wa benki ya National Savings, Pradeep Kariyawasam, pia alikamatwa kwa kuhusishwa na kesi hiyo, licha ya kuwepo nje kwa dhamana.

CHANZO:Anadolu Agency