Rais wa Misri, Abdel Fattah Al Sisi, alisema Jumamosi kwamba muhula wake wa urais utaisha mwaka 2030, akisisitiza kuwa katiba ya nchi hiyo haitafanyiwa marekebisho ili kuongeza muda wake wa kukaa madarakani, kulingana na gazeti la serikali la Al-Ahram.
"Mwaka 2030 utakuwa mwisho wa muhula wangu wa urais. Jambo hili limeamuliwa kabisa," alisema Sisi wakati wa sherehe ya kuhitimu katika Chuo cha Kijeshi cha Misri, kilichopo katika Mji Mkuu Mpya wa Utawala.
Sisi, ambaye alichaguliwa tena kwa muhula mpya wa miaka sita akipata karibu asilimia 90 ya kura mwaka 2023, alisema katiba ya Misri "haitaguswa," akisisitiza umuhimu wa kuzuia ukiukwaji wowote wa kanuni za kikatiba na kidemokrasia.
Alisema katiba inaainisha jukumu la majeshi katika kulinda utaratibu wa kikatiba, demokrasia, na nguzo za msingi za taifa.
Aahidi kuilinda Saudi Arabia
"Sitauacha taifa la Misri hadi pale litakapokuwa limejaa watu wake wenyewe wenye uwezo wa kubeba majukumu," aliongeza, akisema kizazi kipya cha viongozi kinaandaliwa kwa sasa kupitia Chuo cha Kijeshi cha Misri.
Sisi pia alisema Misri iko tayari kuchukua hatua yoyote itakayombwa na Saudi Arabia kwa ajili ya kulinda usalama na mamlaka ya ufalme huo.
"Tutachukua hatua yoyote kulinda Saudi Arabia," alisema, akiongeza kuwa ataliomba bunge kuitisha kikao cha dharura ili kuidhinisha hatua kama hiyo, iwapo ombi litatolewa.
"Tunasimama imara kulinda na kutetea maeneo ya ndugu zetu katika eneo la Ghuba," aliongeza.
AFRIKA
2 dk kusoma
Rais wa Misri asema ataondoka madarakani mwaka 2030, aahidi kutobadilisha katiba
Rais wa Misri, Abdel Fattah Al Sisi, alisema siku ya Jumamosi kuwa muhula wake wa urais utaisha mwaka 2030, akisisitiza kuwa katiba ya nchi hiyo haitafanyiwa marekebisho ili kuongeza muda wake wa kukaa madarakani.

Soma zaidi






















