| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Algeria kuanza kutekeleza hukumu ya kifo kwa wanaochoma misitu, watekaji nyara watoto
Hukumu hiyo ya kifo pia itatekelezwa kwa yeyote atakayechochea, kuhamasisha, kufadhili, kupanga au kushiriki katika uhalifu kama huo.
Algeria kuanza kutekeleza hukumu ya kifo kwa wanaochoma misitu, watekaji nyara watoto
Chini ya sheria hiyo, adhabu ya kifo itatekelezwa kwa yeyote anayeanzisha moto kwa maksudi kwenye misitu, na maeneo yenye miti.

Sheria mpya zinazopendekeza hukumu ya kifo kwa uhalifu wa kuchoma moto misitu na kuteka nyara watoto itaanza kutekelezwa nchini Algeria baada ya kufanyika marekebisho ya ibara, Shirika la Habari la serikali la Algeria limeripoti.

Marekebisho hayo, yaliyoidhinishwa na mabunge yote mawili wiki iliopita, yalichapishwa kwenye Gazeti Rasmi la serikali siku ya Jumatano.

Chini ya sheria hiyo, adhabu ya kifo inatekelezwa kwa yeyote anayeanzisha moto kwa maksudi kwenye misitu, maeneo ya miti, sehemu iliyolimwa au kutolimwa yenye miti au mbao ndani ya misitu.

Vipengele hivyo pia vinaangazia yeyote anayechoma moto “kwa maksudi” majengo ya umma au binafsi kwa kuchochewa, au kwa faida ya taifa la nje au chama, au kama sehemu inayohusisha uhaini au kujihusisha na magenge ya uhalifu.

Utekaji nyara wa watoto

Sheria hiyo inataka hukumu ya kifo kutumika kwa yeyote anayemteka nyara mtoto, kumtesa, kumdhalilisha kingono au kumfanyia vitendo viovu.

Rais Abdelmadjid Tebboune aliagiza kurudishwa kwa hukumu ya kifo kwa uhalifu huo kufuatia matukio ya uchomaji moto misitu mwishoni mwa mwezi Agosti ambapo ilisababisha watu kupoteza maisha na uharibifu wa mali, hasa katika mikoa ya mashariki.

CHANZO:َAA