| Swahili
UTURUKI
1 dk kusoma
Trump azipongeza Uturuki na Pakistan kwa kuipa Saudi Arabia msaada wa kijeshi
Siku ya Jumatatu, Uturuki, Saudi Arabia na Pakistan, zilikubaliana kuanza utekelezaji wa kupelekea vikosi vya kijeshi Saudi Arabia, ikiwa ni hatua za awali za utekelezwaji wa mkataba wa Makkah.
Trump azipongeza Uturuki na Pakistan kwa kuipa Saudi Arabia msaada wa kijeshi
Rais Donald Trump wa Marekani./Picha:Reuters

Rais Donald Trump wa Marekani amepongeza makubaliano ya Uturuki na Pakistan ya kutoa msaada wa kijeshi kwa Saudi Arabia.

Akizungumza kabla ya kuelekea Texas, amepongeza mpango huo, akiuita hatua kubwa.

"Nadhani wanataka kuisaidia Saudia Arabia, na nafikiri ni hatua nzuri sana,” alisema Trump mara baada ya kuulizwa na waandishi wa habari.

Siku ya Jumatatu, Uturuki, Saudi Arabia na Pakistan, zilikubaliana kuanza utekelezaji wa kupelekea vikosi vya kijeshi Saudi Arabia, ikiwa ni hatua za awali za utekelezwaji wa mkataba wa Makkah.

Wakati huo huo, mkataba huo utafikishwa mbele ya wabunge wa bunge la Uturiki, na baadaye utapelekwa Pakistan na Saudia Arabia, kulingana na msemaji wa chama tawala nchini Uturuki, AK.

“Mkataba huo utapelekwa siku chache zijazo,"alisema Omer Celik.

CHANZO:Anadolu Agency